Recent news

Wadau Mbalimbali wakitembelea Banda la TAHLISO hapa Jijini Mbeya katika Maonesho yanayoendelea ya Kilimo, ufugaji na Uvuvi.

TAHLISO Katika Banda Letu tunatoa huduma zifuatazo;
1. Elimu ya Uombaji Mkopo na kutatua changamoto zinazojitokeza wakati wa Uombaji.
2. Elimu na Ushauri katika Maombi ya Vyuo vikuu na Vyuo vya kati.
3. Kuonesha Bunifu za wanafunzi katika teknolojia ya Kilimo.
4. Ufafanuzi wa Majukumu yetu na wadau tunaoshirikiana nao katika kulinda Maslahi ya Mwanafunzi.

Karibuni Sana na Huduma zote hizi zinatolewa bila malipo hapa Viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.